Mkazi wa Mkokozi Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani, Sara Zefhania mzazi wa Happness Rioba ambaye alidaiwa kuzamia kwenye ndege jijini Dar es Salaam na kwenda Zanziba.
Sakata lililokuwa limejitokeza la mtoto aliyezamia ndege kutokea Jijini Dar es salaam hadi Zanziba aliyejitambulisha kwa jina la Karine godfrey limeibua sura mpya baada ya kujikeza kwa mwanamke mmoja mkazi wa Mkuranga wilayani pwani na kudai kuwa mtoto huyo niwakwake.

Mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina la Sarah Zefania, ameeleza kuwa mtoto huyo ni wakwake na anaitwa Happynes Rioba na si Karine Godfrey kama alivyojitambulisha mwenyewe.

Zefania alisema kuwa sio kweli kwamba mtoto huyo alikuwa amezamia ndege kama ambavyo alitangazwa na kituo cha Televisheni, bali ni tabia yake ya kupotea katika mazingira ya kutatanisha ambayo hutokea mara kwa mara.

Mwanamke huyo aliongeza kuwa Hakuna ukweli wowote wa mtoto huyo kusindikizwa na dada yake Airport kupanda ndege bali ni ile tabia yake aliyokuwa nayo ndiyo aliyoitumia.

Alisema kuwa mtoto wake huyo amekuwa na tabia hiyo tangu zamani, na alishawahi kutoweka kwa kupindi cha mwezi mzima. Baada ya mama huyo pamoja na ndugu kuhangaika walifanikiwa kumpata mkoani Mwanza akiwa katika mazingira ya kutatanisha.

Taarifa zilizotufikia leo hii ni kwamba mtoto huyo ametoweka katika nyumba Salama huko Zanziba ambako alikuwa akihifadhiwa. Alipatikana baadaye maeneo ya mbali sana kutoka katika nyumba hiyo aliyokuwa ametunzwa.

"Mtoto huyu anatushangaza sana kwani anapenda kuzungumza na wanyama kuliko binadamu wenzake. Kuna wakati utamkuta anazungumza na paka, na mbwa lakini watu wanapomhoji huwa hazungumzi kitu chochote" alisema mwanamke mmoja anayeishi naye.

Kufuatia tabia hiyo aliyokuwa nayo mtoto ya kutoweka mara kwa mara, askari wa jeshi la polisi wamekataa kukaa na mtoto huyo.

Mtoto huyo atakabidhiwa kwa mama yake mara tu atakapofika hapo Zanziba kumchukua mtoto wake.



 
Top