Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Dk. Seif rshid
Bertha Boniphace (25) mkazi wa Kata ya Karoro-Buserere mkoani
Geita amefariki dunia katika hospitali ya wilaya ya Geita alipokuwa amelazwa baada na kuugua ugonjwa uliokuwa ukifanana na ugonjwa wa Ebora.
Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii kimeeleza kuwa, Bertha Boniphace
alikuwa akisumbuliwa na kutapika, kuharisha damu na kutoka damu sehemu za mdomo
na puani, dalili ambazo zinashabihiana na zile za ugonjwa wa Ebola hali
iliyosababisha watu kufikiria kuwa ameuawa na ugonjwa huo.
Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii imetoa matokeo ya sampuli ziliyopelekwa
Nairobi nchini Kenya kuweza kuchunguza chanzo cha kifo cha Bertha Boniface.
Mganga mkuu wa Hospitali ya Wilaya ya Geita, Dk Adam Sijaona
alieleza matokeo ya sampuli hizo kuwa yanaonesha Bertha hakuwa na maambukizi ya
ugonjwa wa Ebola bali alikuwa anaumwa ugonjwa unaojulikana kitaalamu ‘Chikungunya
Viral Hemorrhagic Fever (VHF)
“Bertha hakuuawa na Ebola kama watu wanavyo dhani, bali ni
ugonjwa ambao unataka kufanana na Ebola. Huu ni ugonjwa wa Kitropic ambao
unaenezwa na mbu aina ya Aedes Aegyti. Aina hii ya mbu ni wachache sana. Na wanapatikana
maeneo yenye unyevunyevu” alieleza Dk Sijaona
Mganga mkuu wa mkoa wa Geita, Dk Joseph Kisala naye alieleza
kuwa ugonjwa huo ni mpya nchini na haujazoeleka barani Afrika. Pia ugonjwa huo
hauna tiba maalumu kama ugonjwa wa Dengue.