Mtoto Mwanaafa mshiriki aliyekuwa mdogo kuliko wote katika mashindano ya TMT ameibuka na ushindi wa shilingi milioni 50, na kuwashinda washiriki wenzake ambao wamemzidi sana kiumri


Katika sherehe za fainali zilizofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam, Mshiriki huyo kutokea kanda ya Kusini (Mtwara) ameibuka na ushindi baada ya kupigiwa kura nyingi na wananchi wa Tanzania kutokana na kufanya vizuri katika kipindi chote cha mashindano hayo.

Vifijo na nderemo viliibuka pale Mwanaafa alipotangazwa kuwa mshindi katika mashindano hayo. Huku akiwa analia na kumtaka mama yake, mtoto huyo alikabidhiwa hundi yenye thamani ya pesa za kitanzania shilingi milioni 50.

Hata hivyo washiriki wote 10 ambao walifanikiwa kuingia fainali, wameonekana kuwa na mabadiliko makubwa sana ukilinganisha na kipindi walipojiunga na mashindano hayo. Hivyo TMT imefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kukuza vipaji vya washiriki hao.


 
Top