Kamanda wa Polisi mkoani Arusha, Liberatul Sabas 
Mtu mmoja anayejishughulisha na biashara jijini Arusha, Olais Metili anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 5o, amekutwa amefariki dunia katika
nyumba ya kulala wageni kwenye hoteli ya Diamond Motel maeneo ya Sakina jana majira ya saa saba mcha.

Mfanya biashara huyo anayemiliki duka la vinyago pamoja na mgahawa mmoja jijini hapo, aliingia na mwanamke hotelini humo kabla ya kukutwa na mauti yake. 

“Marehemu alifika hotelini hapa akiwa ameongozana na mwanamke mmoja, ambaye hatukuweza kumuona muda na namna alipoondoka hotelini hapa” alisema mmoja wa wahudumu wa hoteli hiyo.

"Hapa mtaani kuna wamasai wengi sana ambao wanauza dawa za kuongeza nguvu za kiume, wakati mwingine watumiaji zinaweza kuwaletea madhara kama haya zinapokuwa zinafanya kazi mwilini" alieleza shuhuda mmoja wa tukio hilo

Mwili wa marehemu ambao ulikutwa katika hoteli hiyo jana majira ya saa saba mchana, umechukuliwa na askari polisi kwaajili ya kufanyiwa uchunguzi.
 
Top