Mchezaji wa Klabu ya Simba Imanuel Okwi
Kusajiliwa kwa mchezaji Okwi na klabu ya Simba kumeleta mtazamo tofauti kwa watu, hasa wachezaji pamoja na wapenzi wa soka mbalimbali.
Mchezaji wa klabu ya Simba Issa Rashid maarufu kama Baba
Ubaya, amejikuta akipoteza furaha yake baada ya Okwi kutinga katika klabu hiyo
na kupewa jezi yenye namba 25, ambayo alikuwa anaivaa yeye.
Baba ubaya amesema kuwa namba ya jezi hiyo alikuwa anaipenda
sana kwasababu alikuwa anaitumia kumuenzi baba yake mzazi ambaye kwa
sasa ni marehemu. namba ya jezi hiyo inawakilisha tarehe ya kuzaliwa kwa baba yake. Amesema kuwa amejisikia vibaya sana kunyang’anywa namba yake
hiyo na kupewa mtu mwingine. Hata hivyo amesema kuwa hana jinsi na imebidi
kukubaliana na hali halisi.
Sababu kubwa ya mchezaji Okwi kupewa jezi yenye namba hiyo,
ni kwamba awali alipokuwa akiichezea klabu hiyo alikuwa akivaa jezi yenye namba
hiyo hadi mwaka 2012.
Baba Ubaya aliendelea kuzungumza kuwa, namba hiyo ya jezi
alikuwa akiitumia hata alipokuwa akichezea Mtibwa Shugar kabla ya kujiunga na
Simba. Alimaliza kwa kusema kuwa Pamoja na kwamba ameumia sana lakini hana
jinsi na amekubaliana na hali.
KWA HABARI ZA MICHEZO LIKE UKURASA WETU HAPA>>
KWA HABARI ZA MICHEZO LIKE UKURASA WETU HAPA>>