Ndege hiyo yenye namba za usajili 5Y-SXP iliruka kutoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza Jumapili saa 1:26 usiku ikielekea Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta (JKIA) Kenya ambako ilitakiwa kutua saa 2:36 usiku.
Meneja Uhusiano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), Paschal Shelutete alikiri ndege hiyo kuanguka kwenye hifadhi hiyo na walikuwa katika harakati za kuitafuta.
Mkaguzi Mkuu wa Ajali za Ndege nchini, kutoka Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi, David Nyamwihura alisema ajali hiyo ilitokea takriban maili 20 kutoka Serengeti, katika eneo la Kogatembe na watu wote watatu waliokuwamo wamefariki dunia