Wanawake wanaojihusisha na biashara ya kuuza miili yao (machangudoa) mjini Morogoro wajikuta kitumbua chao kikiingia mchanga mara soko lilivyovunjwa ghafla kwa kuondolewa wateja wao.

Machangudoa hao ambao wamekuwa wakijipatia kipato kwa kufanya biashara hiyo haramu ya kuuza miili yao katika maeneo ya Mwanzo mgumu, kata ya Mwembesongo mjini Morogoro, walikuwa wakifanya biashara hiyo katika maeneo hayo na wateja wao wakubwa ni madereva wa maroli ambayo hupaki maeneo hayo.

Madereva na mautingo wa mroli hayo wamekuwa na tabia ya kuwachukua machangu hao na kufanya nao ngono ndani ya magari yao kisha kutupa kondomu na kuchafua mazingira. Jambo ambalo ni hatari hata kwa afya za watoto wadogo ambao hucheza katika mazingira hayo

Kufuatia wananchi wa eneo hilo kukerwa na tabia hizo, Serikali imechukua jukumu la kuhamisha eneo la kuegeshea maroli hayo na badala yake kupelekwa maeneo ya Tumbi nje kidogo ya mji.

Kitendo cha maegesho ya maroli kuhamishwa na kupelekwa mbali sana kutokea mjini kimeleta shida kwa wafanyabiashara hiyo haramu
 
Top