Mtu mmoja mlemavu wa ngozi anayeishi mjini Morogoro, Damas Valenian (36) amevamiwa na jirani yake Lyimo na kukatwa mapanga.

Katika tukio hilo ambalo limetokea wiki mbili zilizopita, Lymo ambaye ni mfanyabiashara alimvamia nyumbani kwake Damas ambaye ni mlemavu wa ngozi (Albino) na kuanza kumkata mapanga akiwania kumnyofoa masikio.

Katika purukushani hizo Damas aliweza kumtambua mtu huyo kuwa ni jirani yake Lymo. Na kwa bahati nzuri mpwa wake Damas anayeitwa John alifika na kumsaidia mjombaake huku wakipiga kelele kuomba msaada.

Baada ya kufanikiwa kuchomoka katika purukushani hizo Damas alikwenda kwa mjumbe wa mtaa wao, Filemon Gyuna na kupatiwa huduma ya kwanza.

Kulipopambazuka walikwenda kutoa taarifa kituo cha polisi na kupewa jalada la kesi namba MOR/5122/2014 – SHAMBULIZI.

Askari walikwenda nyumbani kwa mtuhumiwa na kumtia hatiani ambako walimfikisha kwenye mikono ya sharia.
 
Top