Kamanda wa polisi Morogoro, Leonard Paul

Watu wanaodhaniwa kuwa majambazi jana usiku majira ya saa 8.30 walifunga barabara ya Morogoro Iringa eneo la njia panda ya Kilosa kwa kuweka magogo na mawe barabarani kisha kuteka magari na kupora mali za watu.



Kwa mujibu wa watu walioshuhudia mkasa huo, walieleza kuwa watekaji hao walikuwa wakirusha mawe na risasi kuvunja vioo vya magari yote ambayo yalifika katika eneo hilo kisha kupora mali.


“Ni siku moja tu imepita tangu askari wamtie mbaroni raia wa Burundi akiwa na vifaa mbalimbali vya kufanyia utekaji” alisema mwejeji mmoja wa Kilosa

Vifaa vyenyewe ambavyo alikutwa navyo mtuhumiwa huyo vilikuwa ni pamja na mnyororo wenye misumari, mabomu ya milipuko, na darubini.

Hikuweza kufahamika kirahisi ni watu wangapi wamejeruhiwa katika ujambazi huwo. Na kamanda wa jeshi la polisi mkoani Morogoro Leonard Paul hakupatikana kutoa maelezo juu ya tukio hilo.
 
Top