Zaidi ya Watu 38 wamefariki dunia papo hapo na wengine 86 kujeruhiwa vibaya katika
ajali iliyotokea leo asubuhi majia ya saa tano maeneo ya Sabasaba nje kidogo
mwa mji wa Musoma.
Ajali hiyo inahusisha Basi la kampuni ya J4 Express lenye
nambari za usajiri T 677 CYC lililokuwa likitokea Mwanza kuelekea Silari mkoani
Mara, na basi la Kampuni ya Mwanza Coach lenye nambari za usajili T 736 AWJ
lililokuwa likitokea Musoma kuelekea Mwanza.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari kilichoripoti, chanzo
cha ajali hiyo ni basi la kampuni ya J4 kujaribu kulipita gari ndogo Nissan
Terano lenye nambari za usajili 332 AKK karibu na daraja ambalo linauwezo wa
kupitisha gari moja.
Kutokana na mwendo kasi wa mabasi yote mawili J4 na Mwanza
Coach, yalishindwa kupishana na kuvaana uso kwa uso yakijumuisha gari ndogo
ambayo ilitumbukia mtoni na kuua watu wawili, mmoja majeruhi.
Majeruhi pamoja na maiti walifikishwa katika hospitali ya
mkoa iliyopo Musoma kwaajili ya huduma pamoja na utambuzi kwa wale waliopoteza
maisha. Hadi ilipofika majira ya saa kumi na moja jioni idadi ya watu walifariki ilikuwa zaidi ya 40
INNALLILLAHI WAINNA ILAIHI RAJIUN – BWANA AMETOA BWANA
AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE