UTAMU WA RAHA INAOMBA RADHI KWA PICHA HIZI
Mwili wa mmoja wa majambazi ukiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti
Baada ya UTAMU WA RAHA kuripoti
taarifa za ujambazi wa kuteka magari uliofanyika katika tarehe 2 Septemba majira ya saa 2:30 usiku maeneo ya Kilosa njia
panda ya Iringa kule Morogoro, watu watano wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wameuawa na
jeshi la polisi mkoani Kigoma katika majibizano Yarisasi.
Kamishna msaidizi wa polisi mkoani
Humo, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa, Tukio hilo limetokea
maeneo ya barabara kuu ya Kasulu Kibondo kwenye pori la Malagalasi majira ya
saa 11 alfajiri Septemba 3 mwaka huu.
Askari wa doria walipata taarifa kuwa
majambazi kutoka Burundi walikuwa na mpango wa kufanya utekeji wa magari katika
eneo hilo. Baada ya askari kupata taarifa hizo walijipanga na kuweka mtego
katika eneo la tukio” alisema Kamanda Ibrahim na kuendelea
Baada ya muda majambazi hao walifika
eneo la tukio kwa malengo ya kukamilisha mipango yao. Hapo ndipo walipoanza
kurushiana risasi na askari polisi.
Jeshi la askari polisi lilifanikiwa
kuwaua majambazi watano na kukamata vifaa vilivyokuwa vimekusudiwa
kutumiwa katika kufanyia uhalifu huo. Vifaa hivyo ni pamoja na mabomu matatu ya
kurusha kwa mkono, silaha za kivita mbili aina ya SMG, pamoja na AK 47, na risasi
64 ” alisema Kamanda Ibrahim.
Miili ya majambazi hao imehifadhiwa
katika hospitali ya wilaya ya Kasulu kwaajili ya Utambulisho.