Ni siku mbili tu zimepita tangu  kuliporipotiwa kutokea ajali mbaya mkoani Mara iliyohusisha mabasi mawili ya abiria kampuni ya J4 na Mwanza Coach yaliyogongana uso kwa uso na kuua zaidi ya watu 35 na kujeruhi 85. Taarifa za ajali nyingine iliyotokea mkoani Mrogoro zimeifikia UTAMU WA RAHA.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro Kamishna msaidizi muandamizi wa polisi (SACP) Faustine Shilongile, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo asubihi ya leo majira ya saa 5 maeneo ya Kiegea wilayani Gairo mkoani humo.

 Ajali hiyo inayohusisha basi la Kampuni ya AIRBUS iliyokuwa ikitokea Dar es salaam kuelekea Tabora imesababisha vifo vya watu wane na kujeruhi wengine zaidi ya 30.

“Wamefariki abiria wanne na wengine zaidi ya 30 wamejeruhiwa. Hata hivyo chanzo cha ajali bado hakijafahamika” alisema Shilogile.

Baadhi ya majeruhi wamefikishwa kwenye hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa matibabu.

  


 
Top