Usajili wa Mchezaji mbrazil, Geilson Santos Santana Jaja katika klabu ya Yang African umegonga mwamba baada ya mchezaji huyo kutaka kulipwa dola za kimarekani 600,000 (Tsh 96o mil)

Kiasi hicho cha pesa kimekuwa ni kikubwa sana kwa timu hiyo. Hivyo uongozi wa Yanga wameamua kutupilia mbali mpango wa kumsajili mchezaji huyo na kumfikiria tena Okwi ambaye wamemsajili kwa pesa nyingi.

Pia uongozi wa timu hiyo umeweka wazi kuwa Jaja hana uwezo kama aliokuwa nao Okwi, hivyo hawana budi kubakia na Okwi na kuachana na Jaja.

Vilevile wameamua kufanya hivyo ili kuhakikisha wanamkomesha Okwi ambaye amekuwa akiwaletea usumbufu kwa muda mrefu.

Hata hivyo baada ya mambo hayo kutokea mchana wa jana, leo hii mchezaji Okwi amechukuliwa rasmi na klabu yake aliyokuwa akichezea zamani Simba Sports Club.

 
 
Top