Picha hii ni Polisi akiwa na Kijana anayetuhumiwa kufanya tukio hilo la kinyama.

Tukio hili la kinyama limetokea nchini Ghana  maeneo ya Techman ambapo kijana mmoja ametiwa mbaroni na jeshi la polisi kwa kosa la kumkata kichwa kijana mwengine. Chanzo cha taarifa hizi kwa mujibu wa mtandao mmoja wa kijamii wa nchini humo kimesema kuwa sababu ya kijana huyo kufanya tukio hilo hazikuweza kufahamika. Hata hivyo tukio hilo linahusishwa na imani za kishirikina ambapo baadhi ya watu hufanya matukio ya namna hiyo kwa tamaa za kujipatia mali harakaharaka pasipo kutoka jasho.
 
Top