Vijana wengi wa kiume huwa na mashaka kwamba
uume wao ni mdogo mno, mrefu mno, mwembamba mno, au mnene mno.
Ukweli ni kwamba hakuana umbo wala ukubwa
maalumu. Ukubwa au umbo lolote ni sawa, ni kawaida.
Wakati kijana wa kiume amedindisha uume wake
huweza kuelekea upande wowote, ama kuangalia kwa juu. Muelekeo wowote ni sawa
tu na wakawaida.
Ukiwa na baridi au ukiwa na wasiwasi damu
inayoingia kwenye uume wako ni ndogo zaidi. Lakini ukiwa na joto ama umetulia,
damu nyingi zaidi huingia kwenye uume hivyo unaweza kuwa mkubwa zaidi.