Mwanamke mmoja aliyetambulika kwa jina moja tu la Mwanaheri amejikuta katika wakati mgumu baada ya kunaswa kwa tuhuma za utapeli Mlimani City jijini Dar es salaam.


Mtuhumiwa Mwanaheri akiwa Chini ya ulinzi wa Polisi

Mwanaheriu anadaiwa kuwatapeli wanawake wenzake ambao wanajihusisha na biashara za Living Vorever jijini humo kwa kuchukua vitu vyenye thamani ya shilingi Milioni mbili.

Mwanamke huyo ambaye aliunganishwa katika kundi hilo la ujasiriamali na mtu anayedaiwa kuwa ni mama yake mdogo, alianza usumbufu mara tu alipokuwa akitakiwa kulipa deni lake.

Wanawake wenzake kila walipokuwa wakimpigia simu Mwanaheri hakuwa anapokea na pale mama yake mdogo alipojaribu kumpigia yeye aliishia kujibu jeuri na kutoa matusi.

Baada ya kuhangaishana naye kwa muda mrefu ndipo wanawake hao walipopata akili ya kumpanga mtego ambao ndio matunda yake yameonekana kwa kumtia mikononi.

Katika mtego huo walimpanga mtu na kujifanya alikuwa na shida ya kufanya naye biashara, ambapo Mwanaheri alikubali na kupanga kukutana naye Mlimani City. Huko ndiko wanawake hao walipombananisha mdeni wao huyo aliyekuwa akiwasumbua kwa muda mrefu.

Baada ya pata shika nguo kuchanika huku watu wakijazana kushangaa tukio hilo, wanawake wakiwa na askari wa Mlimani City walimuingiza Mwanaheri kwenye gari na kuondoka naye kwaajili ya mahojiano kisha kumfikisha kwenye vyombo vya dola.

 ________________________________________________________________________________


 
Top