https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiPYFVtX5fQlDg52SXnkxEzISKxbRESSNopv7J5C_HdIg9bRPOey3PJ3DX-vIyh_fItdxAWl5Yi9Sffn0lo00BUxLRNVeYjbRO_AqDD8Dv1LeCxZJ4zQET71god_gY25hDe2YHpNTpwMgts/s320/00013.jpg

Wanaume wawili ambao majina yao hayakuweza kufahamika kwa urahisi, wamejikuta wakiingia katika wakati mgumu wa kunusuru maisha yao baada ya kutiwa mikononi mwa raia wenye hasira kali kwa tuhuma za kumvamia mwanamke na kumuibia.

Katika tukio hilo chanzo cha habari kimesomeka kuwa baada ya mwanamke aliyeibiwa kupiga yowe na kuomba msaada, wananchi walifanikiwa kuwazingira vibaka hao na kuanza kuwaporomoshea kipondo na kufikia hatua ya kuwamwagia petroli tayari kwa kuwachoma moto.

Hata hivyo wananchi hawakufanikiwa kuwatia moto vibaka hao kwasababu jeshi la polisi walifika na kufanikiwa kutetea uhai wa wahalifu hao. Jeshi la polisi linaomba wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi pindi kunapotokea tukio kama hilo au linalofanana na hilo.

 
Top