Kutokana na tathmini ambayo imefanywa na wataalamu mbalimbali imebainika kuwa ni asilimia 25 tu ya wanawake ambao wanafika kileleni wakati wa kufanya mapenzi ama tendo la ndoa hapa ulimwenguni. Hali hii huweza kusababishwa na mambo mbali mbali kama yafuatayo:
1: Afya ya mwanamke. Ili binadamu yeyote aweze kufurahia
tendo la ndoa ni lazima awe na afya nzuri. Inakuwa ni kitu kigumu sana kwa
mwanamke kuweza kufika safari ya mapenzi endapo afya yake haikubaliani na
ubongo. Hivyo magonjwa huweza kusababisha mtu hasa mwanamke kwa namna moja ama
nyingine kutokufurahia tendo. Kitu cha kufanya ni kuhakikisha mpenzi wako
anafanyiwa uchunguzi wa kibailolojia na kupatiwa matibabu haraka sana
ikibainika kuwa ni mgonjwa.
2.
Jambo la pili ambalo mwanamke ama mtu yeyote anatakiwa kulizingatia ni utayari katika kufanya tendo la ndoa.
Endapo Mwanamke hayupo tayari kufanya tendo hilo ni vigumu kufurahia shughuli
na badala yake mtu wa namna hiyo huambulia maumivu kuanzia mwanzo hadi mwisho
wa shughuli. Hali hii hutokea kwasababu kuna uhusiano mkubwa sana wa ubongo na
hisia za kimapenzi. Endapo utakumbana na hali kama hiyo unatakiwa kufanya kila
namna ambayo mwenzi wako atakuwa tayari kisaikolojia na kimwili kufanya
shughuli husika.
3.
Jambo lingine ambalo huambatana na hili
ni hali ya uchovu. Hili nalo huweza kusababishwa na mizunguuko mingi ama
kufanya kazi nzito ambazo humchosha mwanamke na kumsababishia akili yake
kuchoka pia. Endapo mwanamke atakuwa amechoka ni vigumu sana kwa kumfanya
afurahie tendo. Hali hii si kwa mwanamke
tu bali hata kwa mwanaume pia. Kwahiyo jambo la kufanya ili kuepuka tatizo hili
ni kuhakikisha mwanamke amepumzika vya kutosha kabla ya kuanza shughuli.
4.
Mazingira yanaweza kusababisha mwanamke
asifike safari yake. Kujirudia kwa mazingira ya kufanyia shughuli mara kwa
mara huweza kusababisha mtu kushindwa kufikia safari yake. Imezoeleka kuwa eneo
pekee ambalo kwa kawaida hufaa zaidi kufanyia mahandosi ndi chumbani tena
kitandani pekee. Hali hii huweza kumfanya mwanamke kuzoea mazingira na
kuyachoka pia. Kwa namna hiyo ni vyema kujitahidi kubadilisha mazingira. Kwamfano
kama mmezoea kukutana chumbani basi siku nyingine mahandosi yanaweza kuendelea
hata jikoni, bafuni, ama sitingrum. Ilimradi mazingira yamebadilika. Vilevile
inaweza kuwa ni chumbani lakini isiwe kitandani kama ilivyo mazoea yenu. Pia
unaweza kubadili hata aina ya taa kama ni usiku, unaweza kutumia taa ya rangi
badala ya taa yenye mwanga mkali. Endapo umezoea kutumia chemli basi unaweza
kutumia hata kibatari ama mshumaa. Pia
harufu ya manukato ambayo yanampendeza mwenzi wako yanaweza kuvuta hisia zaidi
na kumfanya kuwa tayari.
5. Kukosekana
kwa maandalizi ya kihisia kabla ya tendo. Hili ni jambo la msingi sana
ambalo linampasa mwanaume
yeyote kulifahamu kabla ya kukutana na mpenzi wake. Kwa mkulima ni lazima
kuandaa shamba kabla ya kupanda, kwa mvuvi ni lazima kuandaa nyavu zake kabla
ya kuingia majini, na kwa muwindani ni lazima kuandaa silaha zake kabla ya
kuingia mawindoni, Halka dhalka kwa mpenzi ni lazima kumuandaa mwenzi wake
kabla ya kuanza shughuli ya kuserebuka.
6.
Mwanaume kuwahi kufika kileleni kabla ya
mwanamke. Katika hili napenda kuweka wazi kuwa wanawake ni tofauti na
wanaume. Wanawake walio wengi huchukua muda mrefu zaidi kuweza kufika mwisho wa
safari. Kwa utafiti iliyofanyika na wataalamu wengi Imebainika
kuwa wanawake walio wengi wanaweza kufika safari ya mahabati kuanzia dakika 45
hadi 60 na kuendelea. Kutokana na hali hiyo wanawake wa namna hiyo wanajikuta
wakiwa katika bahati mbaya siku zote hasa wanapokutana na wanaume ambao wanapiga
bao kila baada ya dakika 10 ama 15.
7.
Mwanamke kukosa maandalizi ya kutosha
kabla ya tendo. Naomba hapa tuelewane kidogo, wanawake hutofautiana kutoka
mmoja na mwingine. Wapo ambao huwa hawachelewi kufika safarini (Mshindo), na
wakati mwingine utakuta wakati wa maandalizi tu wenyewe anakuwa wamekwisha jisevia
mara kadhaa na pindi unapoingia kwenye shughulini unakuwa unamtafutia safari
nyingine. Halka dhalka kuna wanawake wengine si rahisi kuweza kuwapata katiaka
wakati wa maandalizi hasa kama utashindwa kufahamu maeneo nyeti ambayo huweza
kumletea mshawasha na hamasa ya shughuli. Endapo mwanaume utakuwa umefanikiwa
katika kipindi hiki basi hautapita muda mrefu kuweza kumpeleka mwenzio pale
panapostahili.
Kuzoea
staili/ mikao ya kufanya mapenzi. Suala jingine ambalo ni nyeti katika
tendo la ndoa ni matumizi ya staili. Watu walio wengi hasa waafrika wamezoea
staili moja tu ya kifo cha mende, naweza kusema staili hii ni maarufu sana.
Inaaminika kila mtu ambaye amewahi kushiriki katika shughuli hii basi amewahi
kuitumia staili hii.
Kwahiyo Endapo kila unapokutana na
Mchuchu mkao (Staili) inayotumika ni ileile ya kila siku, Lazima kuwepo na
ugumu kwa mwanamke huyo kuweza kufikia safari yake akiwa salama. Hali hii
inamfanya kukuzoea na kukuona yuleyule na hatimaye kukuchoka. Lakini kama
unakuwa ukimbadilishia staili kila mnapokutana, atakuona mpya kila kukicha hata
mkiishi kwa miaka zaidi ya miamoja. Unaweza kutumia staili kama vile Mtwike, mwendochatu,
mwitemwima, kitakobega,mkondonungwi, nk