Basi la kampuni ya Morobest Scania yenye namba za usajili
T258 AVH limepata ajali asubuhi ya siku ya Jumatano baada ya kugongana usokwa
uso na Lori maeneo ya Kongwa mkoani Dodoma.
Katika ajali hiyo imeripotiwa kuwa watu 17 walipoteza maisha
hapohapo na wengine 56 kujeruhiwa vibaya.
Kamanda wa Polisi Mkoani Dodoma amethibitisha kutokea kwa
ajali hiyo na amesema kuwa chanzo chake ni uzembe wa madereva (Dereva wa Lori)
ambapo dereva wa Lori ambaye kwa sasa ni marehemu alikuwa akijaribu kulipita
Lori jingine kabla ya kukutana uso kwa uso na basi hilo la Morobest na
kusababisha vifo vya watu hao na majeruhi.
Marehemu ambao walitambuliwa katika ajali hiyo
ni pamoja na
Dereva wa lori Gabriel Lemanya Mkazi wa Ndebwe wilayani Chamwino,
Dereva wa basi Said Lusogo,
kondakta wa basi Omari Mkubwana,
Mikdadi Zuberi ambaye alikuwa ni utingo wa
Lori.
Wengine ni
Wengine ni
Justin Makasi, Gabriel Chiwipe, Marick Masawe,
Melina Maliseli, Wilson Sudai wote wakazi wa Mpwapwa na watu wawili
waliotambulika kwa jina moja moja ambao ni Christina mkazi wa Mpwapwa na Nasibu
mkazi wa Kongwa.
Miili ya marehemu wote imehifadhiwa katika
hospitali ya wilaya ya Kongwa na wengine katika hospitali ya Mkoa wa Dodoma,
huku majeruhi nao wakilazwa katika hospitali hizo kwa matibabu.