Tunapo
sema tatizo la kufika kileleni tunazungumzia makundi makuu matatu, ambayo ni Kuwahi
kufika kileleni kwa muda mfupi mno, kuchelewa kufika kileleni, na kufika
kileleni kusiko sawa. Matatizo yote haya tunayaelezea hapa chini moja baada ya
jingine.
1. KUCHELEWA KUFIKA KILELENI
Mwanaume
ambaye anatatizo kama hili huwa anachukua muda mrefu sana kufika kieleni wakati
anapofanya mapenzi, au wakati mwingine kushindwa kabisa kufika kileleni hata
kama awe anapenda na anapata hisia katika kufanya mapenzi. Tatizo hili
kitaalamu huitwa Retarded ejaculation
Matibabu yaliyopendekezwa kitaalamu kupatiwa mtu
mwenye tatizo hili la kuchelewa kufika kileleni yanatakiwa yaendane na sababu
ya tatizo lenyewe. Kama inadhaniwa kuwa chanzo chake ni athari za kutumia dawa
Fulani (side effect), kubadilisha dozi na kutumia nyingine kutasaidia kuondoa
tatizo hilo. Lakini kama tatizo linaaminika kuwa limesababishwa na athari za
kisaikolojia, inatakiwa kupewa ushauri wa kisaikolojia.
Wanaume walio wengi hawahitaji kupatiwa huduma ya
matibabu ya tatizo la kuchelewa kufika kileleni kwasababu bado wanao uwezo wa
kufurahia tendo la ndoa, na pia hali hii haina madhara kiafya. Ingawa yapo
matibabu yanayo wezakuondoa tatizo na kumfanya mhusika kufika kileleni.
Hata hivyo kama unahitaji kuwa na watoto na
kuitwa baba basi upo ulazima wa kufanyiwa matibabu haraka.
2. KUFIKA KILELENI KUSIKO KWA KAWAIDA
Aina
hii ya tatizo linatokea wakati mwanaume anapofika kileleni mbegu za
kiume/shahawa zinarudi nyuma na kuingia kwenye kibofu cha mkojo badala ya
kuelekea kwenye mirija ya kutolea shahawa hizo nje.
Mwanaume mwenye tatizo hili
huwa anapofika kileleni anajisikia raha kama wengine lakini yeye mbegu zake hazitoki nje, na kama
zikitoka basi huwa ni chache mno.
Tatizo hili halina madhara yoyote ya
kiafya kwa mwenye nalo, isipokuwa linaweza kumletea ugumba wa mwanaume na
kushindwa kupata mtoto. (Kitaalamu tatizo hili huitwa Retrograde ejaculation
3. TATIZO LA KUWAHI KUFIKA KILELENI
Kitu
cha kwanza kabisa ambacho ningependa kukiweka wazi kwako ni kwamba tatizo hili
la kuwahi kufika kileleni ni janga la kidunia, ambapo mwanaume anajikuta
akifika kileleni mapema sana wakati wa kufanya mapenzi kinyume na kupenda
kwake.
Wanaume
wengi hawaelewi ni muda gani ambao ni wa kawaida wanatakiwa kufika kileleni
wakati wanapokutana na wapenzi wao. Wataalamu waliobobea katika masuala haya
wamefanya uchunguzi wao kwa kutumia wanaume 500 kutoka katika nchi tano (5)
tofauti za hapa ulimwenguni. Umepatikana wastani wa muda ambao hutumiwa na wanaume
kufika kileleni mara tu wanapoingiza uume wao kwenye uke wa wapenzi wao ni kati
ya nusu dakika na dakika tano.
Ingawa
ni jukumu la mtu na mpenzi wake kukaa na kujadili wenyewe kama endapo
wanaridhika ama hawaridhiki kutokana na muda ambao mwanaume anautumia kufika
kileleni, Kwakawaida kufika kileleni kabla ya dakika ama ndani ya dakika moja
mara tu mwanaume anapoingiza uume wake kwenye uke wa mwenziwake, linachukuliwa
ni kama tatizo la na linahitaji kupatiwa ufumbuzi mapema.
Mambo ambayo yanaweza kusababisha tatizo hili la kufika kileleni ni,
· Msongo wa mawazo,
· Migogoro katika mahusiano,
· Mama ulishawahi kupata shida yoyote katika mapenzi siku za awali,
· Kutokuwa na furaha,
· Magonjwa kama vile kwashakoo na mengineyo.
· Baadhi ya wataalamu waliofanya uchunguzi wanadhani kuwa baadhi ya wanaume wanakabiliwa na tatizo hili kutokana na maumbile yao, kama vile kuwa na uume ambao hauna nguvu (Kuzaliwa Hanithi)
· Kufika kileleni kusiko kwa kawaida kunasababishwa na kuharibika kwa mishipa au misuri ambayo inazunguuka kwenye shingo ya kibofu cha mkojo. Uharibifu huu unaweza kusababishwa na kufanyiwa upasuaji wa kibofu cha mkojo