"Habari
za siku hii Bwana na Bibi UTAMU WA RAHA. Mimi ni mvulana mwenye umri wa miaka
kati ya 18 na 21. Mimi ni mwanafunzi wa kidato cha nne katika shule fulani hapa
jijini Dar es Salaam. Kuna kitu ambacho
kimekuwa kikinitatiza sana ndani ya ubongo wangu. Naweza kusema kuwa kwa kiasi
fulani nimejikuta nikipoteza amani juu ya hili. “Hivi ni saizi gani ya ukubwa
wa bunduki ambayo inaweza kumfaa /kumfikisha mwanamke wakati wa uwanja wa sita
kwa sita?”
Habari
za siku ni nzuri ndugu yetu. Kwanza kabisa napenda kuanza na kukupa pole kwa
utata ambao upo nao juu ya suala hili. Hata hivyo dawa ya utata ni kupatiwa
utatuzi ulio sahihi. Jambo la pili ni kwamba ningependa kukupa ushauri juu ya
masuala haya ya mapenzi, kwakuwa bado wewe ni mwanafunzi si vyema kuanza
kujiingiza kwenye masuala kama haya. Nasema hivi kwasababu ni vijana wengi sana
wamejikuta wakifanya vibaya katika masomo yao kwasababu ya mapenzi. Umri wako
bado unaruhusu mdogo wangu, soma kwanza mapenzi yapo hayaishi. Lakini kwakuwa
unautata kichwani mwako si vibaya kama tutautatua kwasababu ni sehemu ya
mafunzo yako. Leo hii unakwenda kuwa huru juu ya utata huwo hasa baada ya
kumaliza kusoma ukurasa huu.
Wanaume
walio wengi wanaamini kuwa ili kuweza kumfikisha mwanamke wakati wa kupeana
mambo yetu ni lazima bunduki husika iwe na ukubwa unaoanzia nchi 8 – 9 na
kuendelea. Pia inaaminika kuwa ni udhaifu mkubwa sana kwa mwanaume kuwa na
bunduki ndogo. Kutokana na imani hii ndiyomaana leo hii kumekuwa na mrundikano wa waganga wa jadi
ambao wanajipatia pesa kwa kudai kuwa wanazo dawa ambazo zinaongeza ukubwa wa
bunduki.
Leo
naomba niweke wazi kuwa saizi ya bunduki haihusiani na kumfikisha mwanamke
katika dunia ya malavidavi. Naweza kusema maneno haya kwasababu mwanamke hapati
raha za mapenzi kwa kuguswa sehemu za ndani kabisa za hazina pekeyake. Kama
ingekuwa iko hivyo ni kwanini mwanamke anapomchezewa anaweza kufika kileleni
pasipo hata kuingiza bunduki yako katika hazina yake? Au unadhani kwa wale
ambao wamekuwa wakijiingiza kwenye ule mchezo mchafu wa Kusagana hizo bunduki
zilizokuwa na ukubwa wa inchi 8 – 9 watazitoa wapi?
Sasa
ni wakati wa kubadilika ndugu yangu, imani juu ya dhana hiyo ambayo mimi naiita
dhana potofu ni vyema ukaifuta kichwani mwako. Sikulazimishi uifute lakini
naomba utambue kuwa kuna baadhi ya wanawake wanakimbia ndoa zao pamoja na
kwamba waume wao wanamiliki mizigo ya kutosha, na kukimbilia kwa wenye bunduki
ndogo. Kazi ni kwako kufikiri juu ya hili.
Kitu ambacho ningependa kifahamike hapa ni
kwamba, kuwa na bunduki ndogo ama kubwa si tatizo la kukufanya upoteze amani
ama ujione dhaifu mbele ya wengine. Isipokuwa tatizo lililokubwa na la kuogopa
ni kutokuwa na nguvu za kutosha katika kusakata mchakato mzima wa sita kwa
sita. Kitu cha msingi na cha kuzingatia ni namna ambavyo wewe mchakalikaji
umejiandaa na umeuandaa vyema mchezo kabla ya mechi kuanza. Unaweza kuwa na
kabunduki kadogo ka ukubwa wa nchi tatu hadi tano lakini mambo yako yakawa
mazito kiasi cha kuleta gumzo mtaani ama kumiliki ndoa yako ipasavyo.