Baada ya mitandao mbalimbali ya kijamii kuripoti habari zinazokinzana juu ya tukio la bwana harusi mtarajiwa aliyetajwa kwa jina la Stephano kunaswa kwenye tukio la ujambazi muda mfupi baada ya kumvisha pete ya uchumba mpenzi wake, Happy Merere. Bi Harusi huyo mtarajiwa ameibuka na kuanika ukweli wa mambo yote.
Kwenye tukio hilo, watuhumiwa hao, akiwemo Stephano au mume mtarajiwa wa Happy waliwekwa chini ya ulinzi na jeshi la polisi.
Baada ya tukio hilo kuthibitishwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam na watuhumiwa Salum Mtamwa, Alex Makunga, Mohammed Ally na Stephano Kikindi kushikiliwa kwa uchunguzi zaidi, watu walianza kuripoti tofauti katika mitandao ya kijamii.Kuna ambao walidai watuhumiwa hao ni majambazi kwa vile walikutwa na bunduki mbili lakini kuna wengine walidai ni vibaka kwa kuwa hawakukutwa na silaha yoyote.
Stephano na Mpenzi wake muda mfupi baada ya kumvisha pete ya uchumba
Wadau wengine kwenye mitandao ya kijamii walijiongeza kwa kudai mtuhumiwa ambaye ni mume mtarajiwa wa Happy wanamjua kwamba anajihusisha na ishu za udokozi hivyo tukio hilo si la kwanza kumtokea.
Happy ambaye awali alianza kukanusha taarifa ambazo zimesambaa kwenye mitandao ya kijamii na kudai nyingi hazina ukweli wowote, alisema:
“Wanajiandikia tu mitandaoni, hakuna ukweli wowote. Eti wanasema mchumba‘angu amekutwa na bunduki mbili wakati taarifa nilizozikuta pale Polisi Central zinasema hawakuwa na silaha.” Alisema Happy kasha akaendelea.
“Wala mchumba‘angu hakuwa jambazi kama watu walivyokuwa wanasema mitandaoni, jalada nililolikuta polisi lilikuwa limeandikwa UNYANG’ANYI na si ujambazi kama wengi walivyokuwa wanavumisha, mimi nimekwenda mwenyewe polisi nikaoneshwa.”
Stephano na wenzake waliponaswa kwenye tukio hilo
Wale watu aliokamatwa nao mchumba wangu ni marafiki zake,
sasa huenda alijikuta amejumlishwa kwenye tukio ambalo halimhusu. Watu
wanazungumza tu pasipo kuwa na ushahidi wowote, mimi mchumba wangu namjua
sijawahi kumuona na viashiria vyovyote vya wizi,” alisema Happy.
Februari, mwaka huu, Happy alivishwa pete na mchumba wake
huyo nyumbani kwao Iringa ambapo mipango ikienda sawa, wawili hao wanatarajiwa
kufunga ndoa hapo baadaye mwaka huu (Mungu akipenda).
Chanzo Risasi