
Mwandishi wa habari hizi alimtafuta mganga huyo kuzungumzia tuhuma
hizo, lakini alikana na kusema kuwa huo ni uzushi. Hata hivyo alikiri wasichana
hao kulala nyumbani kwake.
Mtuhumiwa huyo pia anadaiwa kumjeruhi mfanyakazi wake wa ndani kwa
kumwagia maji ya moto baada ya kumkataa kimapenzi miezi minne iliyopita.
CHANZO: NIPASHE