Wapiganaji wa kundi la Boko Haram kutoka Nigeria wameua watu 38 katika shambulio katika vijiji viwili kusini mwa Niger.
Mbunge wa eneo
hilo, Bullu Mammadu, ameiambia BBC kuwa wanawake na watoto walikuwa miongoni
mwa wale waliopigwa risasi na kuuawa.
Alisema wapiganaji
hao walivishambulia vijiji vya Ungumawo na Lamina Jumatano usiku na kuchoma nyumba
nyingi.
Niger ni miongoni
mwa mataifa yaliobuni kikosi cha kimataifa cha kukabiliana na wapiganaji hao
katika eneo la magharibi mwa Afrika.
Chanzo: BBC