Jaji wa mahakama Moja nchini misri ameamuru polisi aliyepelekwa mahakamani hapo kwa tuhuma za kumuua mwanamke mmoja mwanaharakati wakati wa maandamano mwezi januari awekwe mahabusu.
Tukio hilo
lilisababisha ghasia kubwa nchini humo baada ya video yenye kuonesha kifo cha
mwanahati huyo kusambazwa katika mitandao ya kijamii.
Shaimaa
el-Shabbagh alikufa baada ya kupigwa risasi na askari aliyekuwa ameuficha uso
wake,wakati wa maandamano ya amani katika mji mkuu wa nchi hiyo Cairo mwezi
January mwaka huu .
Picha
video iliyowasilishwa mahakamani na upande wa mashtaka inamwonyesha askari huyo
aliyeuficha uso wake akifyatua risasi upande wa mwanamke huyo kabla
hajabadilisha silaha hiyo na kubeba kifyatua bomu la machozi.
Kuna
madai pia mamlaka zilizuia gari la wagonjwa kuingia ili kumpa huduma
muandamanaji huyo aliyekuwa taabani.
Polisi
nchini Misri kwa muda mrefu wamekuwa ikikana askari wake kutumia risasi za moto
dhidi ya waandamanaji licha ya kuwepo kwa ushahidi mzito unaonyesha wakifanya
hivyo.
Chanzo BBC