Iceland imezua hisia kali wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya usanii katika mji wa Venice nchini Italy baada ya Kulibadilisha kanisa ambalo lilikuwa halitumiki na kuwa msikiti.
Kwa
jina 'La Moschea' msikiti huo unatokana na jengo la santa Maria della
Misericordia,kanisa moja la kikatholiki ambalo lilikodishwa na Iceland na
mwenyewe.
Na
ili kuonyesha uvumilivu wa kidini waislamu wengi walijitokeza kuomba katika
jumba hilo kulingana na chombo cha habari cha AFP.
Wakiwa
wamewacha viatu nje ya lango la jumba hilo,waumini hao walielekea Mecca na
kusujudu huku wageni wakiendelea na ziara zao za za utalii katika jumba hilo.
Uwekaji
wa msikiti huo ulifanywa na msanii mmoja wa Switzerland Christoph Buechel kwa
lengo la kuvutia hisia kutokana na kutokuwepo kwa hata msikiti mmoja katika mji
wa kihistoria wa Venice--mji ulio na uhusiano wa kihistoria na ulimwengu wa
kiislamu.
Lakini
mamlaka ya mji huo imeonyesha kutoridhishwa na hatua hiyo ikisema kuwa jengo
hilo lina hatari ya kushambuliwa na wale wanaopinga Uislamu ama Waislamu wenye
itikadi kali.
Rais
wa jimbo la Veneto Luca Zaia ametaja hatua hiyo kama uchochezi.
Chanzo BBC