Watoto wenye umri wa miaka 10 wanavuta sigara na kula vyakula vyenye mafuta mengi.
Aidha
utafiti uliofanyika Uingereza unaonesha kuwa watoto hao hata wanakunywa
vinywaji vya kuongeza nguvu mwilini kama kiamsha kinywa asubuhi ya siku yao ya
mitihani.
Je wazazi Wanachangia Watoto wao Kuvuta Sigara?
Hayo
ni baadhi tu ya matokeo ya utafiti wa watoto takriban 1,000 uliogundua kuwa 8
kati yao wanavuta sigara asubuhi ya siku ya mtihani.
Utafiti
huo uliofanywa mwaka uliopita uligundua kuwa takriban watoto 37 walikula
Chocoleti kama kiamsha kinywa.
Utafiti
huo uliofanywa na kampuni ya Opinion Matters ilibaini kuwa asilimia 55%
walikuwa wakihofia kuandikisha matokeo duni na kuwa yangeathiri maisha yao ya
baadaye.
Uafiti
mwengine huru uliofanywa wakati huo huo pia uligundua kuwa asili mia 20% ya
wazazi waligundua kuwa watoto wao walishikwa na mhangaiko wakati wa mitihani.
Mzazi
mmoja kati ya nane alisema kuwa wakati huo wa kufanya mitihani, wanawao
walisusia kula kutokana na hofu.
22%
walipoteza usingizi wao mapema kuliko kawaida, 59% walikataa kula wakati wa
mitihani huku 74% ya wazazi wakikiri kushikwa na mahangaiko sawa na hayo wakiwa
wachanga wenyewe.
Watoto wenye miaka 10 wanavuta sigara na kula vyakula vyenye mafuta
Hata
hivyo mwanasaikolojia wa maswala ya watoto Dakta Claire Halsey anasema kuwa sio
jambo la kawaida kwa watoto wachanga hivyo kushikwa na wasiwasi wa mtihani.
''sio
kawaida kwa kweli kuwa mtoto mwenye umri wa miaka 10-11 wanashikwa na hofu
katika mitihani yao''.
Mwenyekiti
wa shirika linahusiana na maswala ya watoto John Coe amependekeza kuwa watoto
wa umri huo wapewe chakula kwa pamoja ilikupunguza shinikizo la matokeo mema.