Inauma sana! katika hali isiyo ya kawaida, Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Martha Masawe (20), mkazi wa Kilakala Mkoani morogoro, ametapeliwa mtoto mchanga mwenye umri wa siku 34 akiwa katika hospitali ya Nunge mjini Morogoro.
Martha Akiwa kwenye Foleni Hospitali

Tukio lililofanywa kimafia lilijiri Ijumaa iliyopita saa 7:00 mchana wakati Martha akiwa kwenye foleni.
Akihojiwa huku akiangua kilio hospitalini hapo Martha alisema:
“Usiku wa kuamkia leo (Ijumaa) mwanagu alikohoa sana, asubuhi baba yake aliniambia nimlete hospitali kucheki kifua.
“Nikiwa kwenye foleni alikuja mama mmoja, akaomba amshike mwanangu huku akisema ni mzuri.
“Baadaye aliniuliza ana tatizo gani? Nikamwambia anaumwa kifua, akanishauri twende dukani tukamnunulie sweta.
 Martha Akilia Kwa uchungu Baada ya Kuibiwa mtoto wake
“Tulikwenda maduka ya Kikundi tukanunua sweta na nguo nyingine kisha kila mtu akapanda bodaboda yake tukaanza safari ya kurudi hospitali.
“Chaajabu nafika hapa hospitali nimekaa zaidi ya nusu saa yule mama hajatokea. Nikawasimulia manesi wakadai tayari nimeibiwa mtoto.”
Baadaye mama huyo alipata msaada wa askari wa doria, afande Mwajabu aliyeongozana naye kwenda kituo cha polisi kufungua mashtaka na namna ya kumuelewesha mumewe.
 
Top