Mshukiwa wa mauaji ya watu tisa katika kanisa moja la kihistoria mjini Carolina Kusini Amekamatwa.
Kulingana na
mwanasheria mkuu Lorreta Lynch,awali maafisa walimtaja kijana huyo wa miaka 21
kuwa Dylann Storm kama mtu waliyekuwa wakimsaka kwa shambulizi la Charleston.
Maafisa wa polisi
wanasema kuwa mshukiwa huyo aliyejihami na bunduki aliketi katika mkutano wa
mafundisho ya biblia kwa takriban saa moja kabla ya kufyatua risasi na kuwaua
wanawake sita na wanaume watatu akiwemo mchungaji wa kanisa hilo.
Maafisa wamelitaja
shambulizi hilo kama la uhalifu wa chuki.
Bi Lynch amesema
idara ya haki itaangazia maswala yote ili kubaini njia mwafaka ya kumfungulia
mashtaka mshukiwa.
Vyombo vya habari vya
Marekani vinasema kuwa bwana Storm alikamatwa huko Selby Carolina kaskazini saa
13 baada ya shambulizi.
Chanzo BBC