Wairi wa kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira, amesema amechukua fomu kugombea Urais ili Kutumia uzoefu wake kusaidia nchi.
Alitoa
kauli hiyo jana mjini hapa alipofika kutafuta wadhamini na kwamba uzoefu
alionao unatokana na kufanya kazi katika serikali zote tangu uhuru
hadi sasa ni nyenzo muhimu kwake kuwania nafasi hiyo kutokana na Taifa
kwa sasa linahitaji mtu anayejua lilikotoka, lilipo na liendako.
Stephen Wasira
“Nimefanya
kazi katika serikali zote hadi sasa, katika serikali ya Rais Kikwete
amepangua na kupangua, lakini hakunipangua, nimekuwa Waziri wa Kilimo, Waziri
Ofisi ya Waziri Mkuu, Waziri katika ofisi ya Rais na hivi karibuni kurudi
Wizara ya Kilimo,” alisema na kuongeza:
“Kubaki
katika nyadhifa zote hizo kwa muda wote ni ishara kuwa mimi nimekuwa na uwezo
wa kufanya kazi na pia kumenisaidia kuijua nchi,” alisema.
Alisema
kujua nchi sio kuijua mipaka bali ni pamoja na kujua maendeleo na matatizo ya
wananchi kwa maelezo kuwa nchi ni watu.
“Nimeamua
nitumie uzoefu wangu na elimu niliyopata kazini tena kwa muda mrefu nisaidie
nchi katika kipindi cha mwaka 2015/20 kwa sababu mazingira ya sasa yanataka mtu
anayejua tulikotoka, tulipo na tuendako,” alisema Wasira.
“Mimi
ninajua tulikotoka mahali tulipo na nina ndoto ya tunakokwenda, na kama hujui
tulikotoka huwezi jua tunakokwenda kwa sababu mtu asiyejua tulikotoka
amekwishapotea maana akitaka kurudi hawezi kujua pa kurudi atarudi wapi?”
alihoji.
Wasira
alisisitiza kuwa uongozi wa nchi unahitaji busara na uzoefu wa kutosha kujua
jambo namna lilivyo.
Mbele ya
makada waliojitokeza kumdhamini, Wasira alitamba kuwa yeye ni msafi, hana
kashifa na kwamba hakusudii kufanya jambo la kashfa.
Chanzo Nipashe