WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Angela Kairuki |
WATUMISHI 12,246 wameondolewa kwenye mfumo wa malipo ya mishahara kwa
sababu mbalimbali, ikiwemo umri wa kustaafu kwa lazima, kufukuzwa kazi,
vifo na kumalizika kwa mikataba.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora),
Angela Kairuki alisema kuondolewa kwa watumishi hao kumeokoa Sh bilioni
25 ambazo zingelipwa kwa watumishi hao.
Alisema kuwa fedha hizo zingepotea endapo watumishi wasingeondolewa
kwenye mfumo, ikilinganishwa na watumishi 10, 295 walioondolewa kwenye
mfumo kuanzia Machi 15 hadi Aprili 30 mwaka huu.
“Jumla ya Sh bilioni 23.2 ziliokolewa kwa kipindi cha Machi 15 hadi
Aprili 30 mwaka huu baada ya Rais John Magufuli kutoa maagizo ya
kuwaondoa watumishi hao kwenye malipo,” alisema Kairuki. Alisema pia
kuwa watumishi hewa 1,951 wameongezeka ikiwa ni pamoja na Sh bilioni
1.8.
Alifafanua kuwa ofisi hiyo ilitoa maelekezo kwa Makatibu Wakuu, Wakuu
wa taasisi za umma na Mamlaka za Serikali za Mitaa, kuwasilisha taarifa
ya watumishi hewa ifikapo juzi (Juni 10 mwaka huu).
Alisema kuwa walielekeza taarifa zibainishe majina, namba za hundi za
watumishi hewa, tarehe walizotakiwa kuondolewa kwenye mfumo, kiasi cha
fedha kilichopotea na kilichookolewa.
Akizungumzia maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma,