Lile jinamizi la Ajali nchini mwetu bado linaonekana kuumiza vichwa vya wananchi na kuongeza hali ya woga na wasiwasi wakati wa kusafiri kutoka eneo moja kwenda eneo lingine haijalishi ni umbali wa namna gani.
Ajali mbaya imeripotiwa kutokea leo eneo la Uwanja wa ndege Kiwira wilayani Rungwe mkoani Mbeya na kuuwa watu zaidi ya 10 baada ya Hiace kutumbukia mtoni.
Wananchi wakiwa katika harakati zauokoaji
Hadi mtoa taarifa wetu alipokuwa akiripoti ilikuwa imebainika kuwa wamenusurika watu wawili tu akiwemo kondakta wa Hiace hiyo.
Wananchi wakiwa katika harakati zauokoaji
Kwa mujibu wa chanzo chetu kimeeleza kuwa Hice zimeanza kufanya safari hizo baada ya Costa zilizokuwa zikifanya safari zake kati ya Kyela na Mbeya Kugoma.