Tukio lilitokea hivi karibuni mkoani Mara la mama wa kambo kumchinja mtoto wake kwa kutumia panga hadi kufariki, limechukua sura mpya baada ya mama huyo nae kushambuliwa na wananchi wenye hasira kali kwa kukatwa katwa na mapanga mpaka kufariki.

Tukio la kukatwa katwa mapanga mama huyo limetokea baada ya wananchi wa kijijini hapo walioshikwa na jazba kali kwa kutokubaliana na kitendo cha kinyama alichomfanyia mtoto huyo kwa kumkatishia maisha yake.

Hata hivyo wananchi walionekana kujichukulia hatua mikononi kwa kumuua mama huyo, kwa kile kilichodaiwa hawakuona hatua zozote za kisheria alizochukuliwa mtuhumuwa huyo kwa kitendo cha kinyama alichokifanya. 

Awali mwenyekiti wa kijiji alifatwa na wanakijiji kuulizwa ni hatua gani ya kisheria mtuhumiwa atachukuliwa kwa mauaji ya kinyama aliyoyafanya kwamaana baada ya tukio, mtuhumiwa alionekana kutochukuliwa hatua yeyote ya kisheria kwa muda mrefu licha ya serikali ya kijiji na polisi kupata taarifa ya kutokea tukio hilo.

Mwenyekiti wa kijiji aliwajibu wanakijiji kuwa polisi wanatambua kutokea kwa tukio hilo na watakuja kumkamata mtuhumiwa na hatua za kisheria za mauaju zote zitafata juu yake.

Muda ulizidi kutokomea bila kuonekana dalili zozote za mtuhumiwa huyo kuchuliwa hatua, ndio wanakijiji wenye hasira kali walipomvamia mama huyo na kumkatakata kwa mapanga kulipiza kisasi kwa kile alichomfanyia mtoto wake.

Mwenyekiti wa kijiji analilaumu jeshi la polisi kwa kuchelewa kumchukua hatua mtuhumuwa mpaka maafa makubwa mengine kutokea.

 

 Picha zikionesha Tukio lilivyoku

SOURCE: Mwanamalunde

 
Top