
Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro
Leonard Paul
Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja
mkazi wa kijiji cha Kindo wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro amefariki dunia
baada ya kunyongwa na baba yake wa kambo kufuatia migogoro ya kifamilia kati
yake na mkewe.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro
Leonard Paul amesema mtoto Abdallah Hamis amenyongwa na baba yake wa kambo
Zamili Shabani (27) muda mfupi baada ya mama wa mtoto kwenda dukani kununua
mahitaji na aliporejea aliingia chumbani kumwamsha mtoto ndipo akagundua kuwa
mtoto amekufa ambapo mtuhumiwa kwa wasiwasi alianza kukimbia na mama huyo
alipiga kelele ya kuomba msaada kwa majirani hadi alipokamatwa.
Mtuhumiwa amekamatwa na atafikishwa mahakamani kwaajili ya kujibu shitaka.
Crdt: Malunde