Mamilioni ya watu wenye asili ya China, duniani kote wanasheherekea mwaka mpya wa kiChina.
Baruti nyingi zilirushwa angani mjini Beijing ikiwa ni ishara
ya kusheherekea siku ya kwanza ya mwaka mpya wa nyani,Nyani wakiwa ni
miongoni mwa wanyama kumi na mbili wanaotumiwa kati ya alama za kichina
katika masuala ya utabiri.
Nako mjini Yokohama nchini Japan, wao
wanasheherekea siku kuu hii kwa kuhesabu muda huku wakicheza ngoma ya
asili ya kucheza na simba.
Maadhimisho ya sherehe hizi za mwaka
mpya zinajumuisha watu kula pamoja,kufanya usafi na familia kuwa pamoja
huku wakirusha fashi fashi angani.
Chanzo: BBC