Raia wa Tanzania ameuawa na umati mjini Nairobi baada yake kuwashambulia na kuwaua watu wawili katika kasino.
Watu walioshuhudia tukio hilo wanasema mwanamume huyo alikuwa amepoteza $300 akicheza kamari.
Alijaribu
kumsihi msimamizi wa kasino hiyo aruhusiwe kuweka rehani simu yake
lakini akakatazwa kwa msingi kuwa haikuwa imefikisha thamani ya kuwekwa
rehani, walioshuhudia wanasema.
Ni hapo ambapo anadaiwa kumdunga kisu msimamizi huyo wa kasino mtaa wa Eastleigh
Mlinzi wa msimamizi huyo alipomkabili, naye pia akamdunga kisu na kumuua.
Baadaye alizidiwa nguvu na umati na kuuawa.
Polisi
wamesema mwanamume huyo ambaye ametambuliwa kama John Barnabas mwenye
umri wa miaka 28 anatoka eneo la Rombo, mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania.
Chanzo: BBC