Je unamkumbuka mwanamuziki wa kufoka Andre Johnson ambaye
alikata Uume wake mwezi Aprili na kisha kujirusha kutoka juu ya jumba moja
mjini Los Angeles?
Sasa basi emetoa sababu zake akisema alikuwa na akili timamu alipokuwa anafanya
hivyo.
Johnson, aliishangaza jamii ya wanamuziki wa kizazi kipya, kufuatia kitendo
chake cha kukata uume wake Kaskazini mwa Hollywood mwezi Aprili. Madaktari
walishindwa kunguanisha sehemu aliyoikata na sehemu nyeti ya mwili wake.
Tangu hapo alikimya kwa miezi miwili akipokea matibabu.
Lakini aliamua wiki hii kujieleza kwa nini alichukua hatua hiyo na kuambia
kituo cha televisheni cha E! nchini Marekani:''Ndio nilikuwa nimetumia dawa za
kulevya , lakini nilikuwa najifahamu.''
'Mimi sio mwanadamu'
Nilikata sehemu yangu ya siri kwa sababu hiyo ndiyo ilikuwa chanzo cha
masaibu yangu. Suluhu langu kwa masaiibu yangu ni kwamba nimeelewa kuwa kitendo
cha ngono ni cha mwanadamu, mimi sio mwanadamu, 'mini ni
mungu''.......''vitendo vya ngono viliniingiza katika matatizo mengi. Mimi siko
hapa ardhini kama mwanadamu bali mungu ''
Matamshi yake Johnson, yanaonekana kama ya mtu anayekabiliwa na matatizo ya
kiakili, lakini Johnson anasisitiza kuwa yuko timamu , yeye sio kichaa.
Alisema amekuwa akipata matibabu ya kisaikolojia lakini daktari alimwambia
hana matatizo.
''Watu wananiona kama mimi ni mwendawazimu, kwa hivyo sikutaka kuongea sana
kuhusu swala hilo. ''
"sikutaka kujiua ,'' alisema Johnson.''
"hilo ndilo jibu langu kwa kitendo nilichokifanya. Leo nafurahi niko
hai, na hilo ndilo jambo muhimu zaidi, hata bila ya uume wangu. ''