https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgjqYCyJhBJZz8ic-AGoXRuQOsbYN_PviVKbB5TA0sP6M2FRrQDCZOnMjQVvZxQ6KYmyRqGp6qHyD3KEnpcbOwuB8hMfyppQXzGyYdkXQ7ahm1HT1ocGLgc2dSv9ItsED0QiVpoxw-6lva_/s1600/20140723_084815_resized.jpg                                                      
Katika hali ya kusikitisha leo Jumatano mnamo majira ya asubuhi, moto mkubwa umezuka katika mabweni ya kulala wanafunzi ya shule ya sekondari Elikisongo wilayani Monduli.


Wanafunzi zaidi ya 100 walionusurika kufa katika ajali hiyo, walikuwa darasani wakati moto ulipozuka ambao chanzo chake inasemekana kuwa ni hitilafu ya umeme. Kwa namna hiyo hakuna mtu ambaye amejeruhiwa na moto huwo, isipokuwa mali ambayo idadi yake bado haijafahamika imeteketea.

Kikosi cha zimamoto kilipowasili katoka eneo la tukio kutokea Arusha na kukuta tayari bweni hilo limekwishateketea kwa moto huwo.

Mbunge wa jimbo la Monduli Mheshimiwa Edward Lowasa alifika eneo la tukio na kuahidi kuwasafirisha wanafunzi kurudi majumbani kwao. gharama za kusafirisha wanafunzi hao ni shilingi za kitanzania laki tano (500,000/=)

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjQ7LCWYEVdYuUOAQEv9tfoYko88VU2n41Zp1jwB64mc2kGkfIrzuMPxSZYbqw2X4mXIKI9eocGJMyYksqQvQNhCKbqDt7K0ln1C3d3wtmexpDGwNwpM3qyiN_0CRZ0r22hVsbQ5utV9uN0/s1600/photo+1.JPG   
 
Top