https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiqpuQURAnwAE2lFX7476J4idFMLjsePQDyj_FJll5DT2ABNvK1JoFVlZybUXM4AyvW8K5dsfPMsO3FYoI_TSDAUXvgYtyE0pOHiiwPmLXKcvqEkAwaNrxem4aPxOuVfKrWDXczRiv-rUdM/s1600/VOT4.jpg
Baada ya kukamatwa kwa mtu anayejifanya daktari katika hospitali ya rufaa mjini Mrogoro siku kadhaa zilizopita, na sasa amekamatwa kijana mwengine mkoani Tabora aliyefahamika
kwa jina la Musa Mbeko (24) aliyekuwa akijifanya ni afisa wa usalama wa taifa.

Kijana huyo ambaye inasemekana kuwa alikwisha wahi kuwa mwandishi wa habari katika redio moja mkoani humo, ametiwa mbaroni na jeshi la bolisi na kitambulisho ambacho kilikuwa kikimtambulisha kuwa yeye ni afisa wa idara hiyo, kwenye kitambulisho hicho kumekutwa jina la Moses R. Kyomo kikiwa na picha yake, kama kinavyo onekana pichani.
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjjlsbjjA0hyphenhyphenZXTsAsnoMgMliWz2FEgxkWu2wV7qzSMh4_RbymByS1GED1o-w_7y7xwrT9x1NXzahLGjobyAyt_YgjkPvDFXCigDqaLdAnWfkvXQsE55fBt-5nQtLWYDuLgIuGFS64KpsRA/s1600/VOT3.jpg

Baada ya mahojiano na jeshi la polisi, Musa Mbeko amekiri kufanya udanganyifu huwo na kutumia kitambulisho hicho kwa utapeli. Jeshi la polisi linamshikilia kijana huyo (musa Mbeko) kwa uchunguzi zaidi.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjOYWQcK7TA8uYEs1afGlcXuMX95hgeQx6n9rxwD67NsDcWiLXPcj-gikvQSYYCJIBncpVSim23Ud0_mi9ljyIm20KNYXUPdnfW4s1lXdlN-V9wfCfGFOWSsZ0xKImEyHR9w82nDqNdYONs/s1600/VOT6.jpg   



 
Top