1. Mtegemezi Kupindukia
Unakuta
mtu anakuwa tegemezi kwa kila jambo hata kama ni kitu kidogo sana
amekipenda dukani basi atakupigia simu ili umnunulie. Anakutegemea
katika kutoa maamuzi ya kila kitu na hawezi kufanya jambo pasipo
kukuomba ushauri hata kama jambo sio zito sana.
Hakuna
kitu
kibaya katika kufanya maamuzi pamoja au mwanaume kumsaidia mpenzi wake
wake kununua vitu lakini sio sahihi kutegemea kwa kila kitu. Mke
anahitaji kuwa huru. Kuwa na uwezo wa kuendesha nyumbani
wakati mume wake hayupo nyumbani na kufanya maamuzi muhimu wakati yeye
mwanaume yupo bize.Mwanamke bora ni yule aliye huru na asiye tegemezi
kupindukia.
2. Mavazi yake
Mwanamke anayefaa kuoa ni yule ambaye anavaa mavazi yenye staha hata
kabla ya kuingia kwenye ndoa. Asikwambie heti atabadilika mara tu
utakapomuoa, bali anatakiwa kubadilika sasa kabla ya ndoa.
Kama
mwanamke yeye anavaa nguo utafikiri za wanamitindo kwenye runinga ama
wacheza filamu, ni lazima abadilike na kuwa mwanamke mwenye maadili ili
hata ifikapo kesho na kesho kutwa watoto wako wasije wakamshangaa ni
kwanini mama yao anavaa vinguo vya ajabu ambavyo ni tofauti kabisa na
maadili ya mwafrika.
3. Mwanamke asiye na Heshima-
Kwa kawaida wanaume walio wengi wanapenda sana kuwa na mwanamke
anayemheshimu awe mpenzi ama mke. Mwanamke mwema ni yule ambaye anajua
kumheshimu kila mtu, awe mwanaume wake ana mtu mwingine yeyote yule.
Kama mpenzi wako hana sifa hiyo kuwa makini, hafai kuwa mke.
4. Mwanamke anayeshindwa kuzuia Hasira zake
- kama ni mwanamke mwenye heshima na nidhamu nzuri, lakini anabadilika
wakati wowote mambo yanapokuwa tofauti na kupoteza heshima yake na
kufanya vitendo visivyo na maadili, yaani mwanamke ambaye anabadilika
badilika kama kinyonga, kuwa makini sana kwasababu ndoa ni kitu kizito
sana ambacho kinahitaji uvumilivu wa hali ya juu.
5.
Muongo muongo-
Wanawake waongo waongo ni wabaya sana. Kama umebaini kuwa mara kwa mara
anakudanganya katika mambo mbalimbali, kimbia haraka sana na uachane
naye mapema. Mwanamke wa aina hiyo hafai kuwa mke mwema.
6. Mnatofautiana katika mambo mbalimbali
- Kama mwanamke yupo tofauti kabisa na vitu ambavyo unavipenda na
kuvipenda vile ambavyo wewe unavichukia ni wazi hamuendani. Ni wazi mtu
wa namna hiyo mtakuwa mnadanganyana na hata kama mkioana basi humo ndani
ya ndoa moto utawaka kila mara.
7. Anatamani kumiliki Kila kitu
- Mwanamke ambaye yupo tayari kununua wave kwa bei ghali kuliko kutumia
pesa katika mambo ya maendeleo huyo hafai kuwa mke bora. Yeye hajali
pesa kama zinapatikana kwa wasiwasi ama laa. Anachoangalia yeye ni
matumizi ya pesa tu. Atatamani kutembelea gari zuri la gharama kuliko
kufanya vitu vingine vya maendeleo.