Mkulima wa kijiji cha Waama. wilayani Hanang' mkoani Manyara, Paschal Yoya amehukumiwa jela miaka 30 baada ya kupatikana na hatia ya kufanya mapenzi na mtoto wake.
Mkulima huyo anadaiwa kufanya unyama huo na binti huyo (jina linahifadhi) katika nyumba ya kulala wageni.
Katika hukumu ya kesi hiyo namba 90 ya mwaka 2013,
Hakimu wa Mahakama ya Mkoa wa Manyara, Gabriel Ngaeje alisema mtuhumiwa
amepatikana na hatia dhidi ya Kifungu cha 158, Kifungu Kidogo cha 1
(b).
Awali, Mwendesha Mashtaka wa Polisi, Wandiba
Wambura alidai Mahakama kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo Septemba 23,
mwaka 2013 kwenye chumba E cha nyumba ya kulala wageni ya California
iliyopo Katesh.
Wandiba alisema kuwa siku ya tukio, Yoya alitoka
na watoto wake watatu kwenye kijiji hicho na kwenda Kijiji cha Gitting
kumsalimu mjomba wao.
“Baada ya kupanga chumba, aliwanunulia chakula watoto wake na baadaye kuwataka kulala bila nguo,” alidai Wandiba.
Alidai kuwa baada ya watoto wengine kualala, alimtaka binti yake kuvua nguo, jambo ambalo binti huyo hakukubaliana nalo.
“Alipokataa kuvua nguo, baba yake alimvua kwa
nguvu na kumtishia kama atakataa kufanya anachotaka atamuua kama
alivyofanya kwa mama yake mwaka 2007,” alisema.
Aliendelea kudai kuwa Agosti 29, mwaka 2013 mtoto
huyo alimweleza mama yake mkubwa kuwa alibakwa na baba yake, ndipo
walipokwenda kutoa taarifa polisi na mshtakiwa kukamatwa na baadaye
kufikishwa Mahakama kujibu mashtaka ya ubakaji.
Chanzo mwananchi
MATUKIO YA KUSISIMUA ZAIDI BOFYA HAPA>>
Chanzo mwananchi
MATUKIO YA KUSISIMUA ZAIDI BOFYA HAPA>>