Katika hali ya kushangaza mwanamke mmoja, Pili Danji Mlapakolo amedaiwa kukutwa akifukia mayai viza kwenye dirisha la dada yake Hanifa Danji Mlapakolo kwenye nyumba wanayoishi iliyopo mtaa wa Kisogo, Kata ya Kiwanja cha Ndege Mkoani hapa.
Tukio hilo
lilitokea Juni 15, mwaka huu saa 11 alfajiri na kusababisha vurugu kubwa kati
ya Hanifa na mdogo wake Pili, jambo lililosababisha umati wa watu kufurika eneo
la tukio wakiwemo ndugu wengine wa familia hiyo.
Dada mkubwa wa
ndugu hao, Saida Danji Mlapakolo ambaye ni mtoto wa kwanza katika familia hiyo
baada ya kuona wadogo zake wamekamatana uchawi aliamua kwenda kuomba ushauri
kwa baba yao mdogo aitwaye Rajabu Mlapakolo ambaye alimshauri kwenda serikali
ya mtaa kwa kuwa yeye alikuwa mgonjwa.
“Ni kweli mdogo
wangu Pili alifumwa na mpangaji wetu akifukia mayai viza na kitambaa cheusi
kwenye dirisha la chumba cha marehemu baba ambacho kwa sasa anaishi Hanifa,”
alisema Saida na kuongeza kuwa nyumba hiyo wanaishi wapangaji na wadogo zake
hao wawili.
Mwenyekiti wa Mtaa
wa Kisogo, Salum Shaban alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na alisema
waliitisha kikao ambapo Pili alipoulizwa alikiri kuchimbia vitu hivyo.“Baada ya
majadiliano nilimuamuru Pili akavitoe vitu hivyo na akatekeleza, hivyo sasa
amani imerejea.
Naye Pili
alipoulizwa kuhusu sakata hilo alisema: “Ni kweli niliweka vitu hivyo ikiwa ni
kinga yangu na wanangu kwa sababu dada yangu naye alikuja na mganga wakazunguka
nyumba bila kunishirikisha.”
Hata hivyo, kauli
hiyo ilimchefua Hanifa ambaye alisema kama ni kinga yake kwa nini asiweka
kwenye dirisha lake?
Katika hatua nyingine siku iliyofuta ndugu mwingine wa familia hiyo, Fatuma Danji Mlapakolo anayeishi Sultan Area alimsihi mwandishi wetu asitoe habari hiyo gazetini kwa madai kuwa baba yao alikuwa maarufu sana hapo mjini, hivyo ikitoka itakuwa aibu kwao.
Katika hatua nyingine siku iliyofuta ndugu mwingine wa familia hiyo, Fatuma Danji Mlapakolo anayeishi Sultan Area alimsihi mwandishi wetu asitoe habari hiyo gazetini kwa madai kuwa baba yao alikuwa maarufu sana hapo mjini, hivyo ikitoka itakuwa aibu kwao.
Chanzo: Ijumaa