Yule mwanamuziki ambaye ameponea chupuchupu kuaga dunia kwaajili ya matumizi ya madawa ya kulevya Rehema Chalamila (RAY C) ameamua kuja na mpango kabambe wa kuwashughulikia vijana walioathirika na matumizi ya madawa hayo.
Ray C amesema kuwa kwa kupitia chini ya kampuni yake ya Ray C Foundation, wanampango wa kuanzisha kituo ambacho kitakuwa kinapokea waathirika wa madawa ya kulevya, ambapo kwa kutumia wataalamu ambao watakuwa wameajiria vijana hao watapatiwa ushauri na matibabu ya kisaikolojia.
Vilevile Ray C amesema kuwa watakuwa wakipita mashuleni kutoa elimu juu ya matumizi ya madawa ya kulevya kwa wanafunzi. Pia ameeleza kuwa watakuwa wakifanya mabonanza mbalimbali kwaajili ya kutoa elimu hiyo mashuleni.