Paul Lambert anatamani kuendelea kubaki Aston Villa hata kama mmiliki wa timu hiyo Randy Lerner atauza Klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Kulingana na taarifa zilizokuwa zimesikika wiki kadhaa zilizopita ni kwamba Mmarekani anaweza kujivua kutoka Klabu hiyo aliyoinunua mwaka 2006.

Kuuzwa kwa klabu hiyo kunaweza kumletea utata Lambat hapo mbeleni, hata hivyo Scot ametoa kauli yake na kusema kuwa matamanio yake ni kubaki Villa hata kama kutokee jambo gani hapo baadae.




 
Top