Bifu kali limeibuka kati ya wasanii wawili wa tasnia ya filamu Wema Sepetu na Kajala Masanja kiasi cha kukaribia kutiana ngumi. Inasemekena kuwa bifu hilo limekuwa kidogokidogo hadi kufikia hatua ya kutishia usalama wao kwa sasa. 

Wema sepetu akizungumza na mwanandishi wa gazeti moja lililotoka ijumaa tarehe 25 amesema kuwa, kajala amekuwa akimfanyia vituko kila kukicha licha ya kwamba yeye (wema) hakuwa anavijali. Anaendelea kusema kuwa Hatosahau siku alipokutana na Kajala kwenye saluni moja na kumkimbilia kumkumbatia kwa shauku kutokana na kuto kuonana siku nyingi. Wema amesema kuwa Kajala alimkwepa na kumtolea maneno machafu huku akidai heti Wema atamchafua. Kutokana na matusi yaliyokuwa yakitolewa na Kalaja, Wema alishindwa kuvumilia na kuporomosha ya kwake jambo ambalo lilisababisha vurugu ya kukata na shoka saluni hapo. 

 
Picha hii ni Kajala na Wema siku Kajala alipoachiwa huru.


 
Top