Mgogoro ambao umeibuka ukiwahusisha wasanii wawili wa Filamu nchini Wema sepetu na Kajala masanja umekuwa gumzo kila kona huku mashabiki wao wakiamini kuwa wawili hao wanagombana kwasababu ya mwanaume (Clement). Jambo ambalo limepelekea wasanii hao kurushiana maneno makali kila kukicha kwenye mitandao, magazeti na hata Televisheni naredioni.
Kukua kwa mgogoro huo kumepelekea wachunguzi wa mastaa kufanya uchunguzi wao juu ya chanzo halisi cha ugomvi huwo ambao chanzo chake hakionekani kuwa na mwanzo wala mwisho.
Kutokana na chanzo cha taarifa hizi, imebainika kuwa kitu kinachogombaniwa na wasanii hao wawili ni mapenzi na si kingine, lakini mapenzi yenyewe ni ya jinsia moja.
Siku za sherehe za kumkaribisha Kajala uraiani baada ya kuachiliwa huru kutoka gerezani zilionekana picha za Kajala akibusiana midomo na Anti Ezekiel. Baada ya miezi kadhaa Ant Ezekiel na Wema walipiga picha wakibusiana na kuzitupia mtandaoni, na baada ya hapo bifu ndio likaanza kuchipua na kukomaa.
KWENYE PICHA NI KAJALA NA ANTI EZEKIEL WAKIPIGANA MABUSU YA MDOMO
Katika picha Wema akimbusu Anti Ezekiel