Basi la abiria la kampuni ya Dar Express limepata ajali masaa machache yaliyopita leo tarehe 9 May 2014 likiwa katika safari zake kutokea jijini Dar es salaam kuelekea jijini Nairobi nchini Kenya.jijini Dar es salaam kuelekea jijini Nairobi nchini Kenya. Basi hilo limepata ajali maeneo ya Msata karibu na Wami baada ya tairi lake la mbele upande wa kushoto kupasuka. Abiria zaidi ya 60 waliokuwemo kwenye basi hilo wamenusurika kufa na kupata majeraha.