Kiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakar Shekau
Wasichana waliotekwa nchini Nigeria na kundi la maharamia
linalofahamika kama BOKO HARAM bado
wameshikiliwa na maharamia hao. Kwa mujibu wa mtandao mmoja wa kijamii wa
Nigeria kati ya wasichana 253 waliokuwa wametekwa nyara, wasichana 53 walifanikiwa
kutoroka na kuwaacha 200 chini ulinzi wa
kundi hilo.
Kundi la Boko Haram limekiri kuhusika na tukio hilo la
utekaji nyara wa wasichana wa nchini humo. Kwa kusisitiza kuhusika kwao katika
tukio hilo Kiongozi wa kundi hilo ametuma kanda ya video . na kwa kuondezea kindi hilo limeahidi kuwauza wasichana hao.
Wasichana hao walitekwa walipokuwa katika shule moja iliyopo
Kaskazini Mashariki mwa nchi wakijiandaa kwa mitihani yao.
Takribani watu 1500 wameuawa na kundi hilo kwa madai kuwa
wanapigana dhidi ya elimu ya kimagharibi. Harakati hizo zilianza tangu mwaka
2009 katika jimbo la Borno.
Maandamano yanayofanywa na wananchi wa Nigeria kupinga utekaji nyara kwa wasichana