PICHANI NI WATU WAKIWA NA MABANGO YAO KUPINGA KITENDO CHA UTEKWAJI WA WASICHANA
Kufuatia kutekwa nyara kwa wasichana zaidi ya 200 nchini
Nigeria na kundi la maharamia lijulikanalo kama Boko Haramu, serikali ya
Marekani imeamua kuingilia kati suala hilo na kutuma wanajeshi wake pamoja na
wataalamu kwaajili ya kuwaokoa wasichana hao.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. John Kery amesema
kuwa Marekani itafanya kila iwezalo ili kufanikisha zoezi la kuwaokoa wasichana
zaidi ya 200 waliotekwa nyara na kundi la Boko Haramu.