Kufuatia aina ya uhalifu uliozuka hivi karibubuni wa watu kufanya matukio yao ya kihalifu kwa kutumia usafiri wa pikipiki na kusababisha madereva wa bodaboda kubeba lawama hizo.
Wahalifu hao wamekuwa wakiwapora watu vitu vyao kama vile mikoba, simu nk, kisha kutokomea navyo kwa kutumia usafiri wa pikipiki. Mbinu hiyo imewawia rahisi wahalifu wanaoitumia kwasababu kukamatwa kwao imekuwa vigumu. Wengi waliofanyiwa uhalifu huwo wamebakia wakilia huku wakiwatazama wahalifu wakitokomea.
Wafanya biashara wa kusafirisha abiria kwa pikipiki wamechoshwa na lawama hizo wanazobebeshwa hivyo wamejipanga kuwa mstari wa mbele kutokomeza tabia ya watu wanaowachafulia jina.
"Tumechoshwa na lawama hizi ambazo zinatuandama kwasababu ya watu wapuuzi. Na tumepanga kutokomeza kabisa tabia hii. Tumebadilishana namba za simu kila kijiwe cha bodaboda, na endapo kutatokea mhalifu ameharibu na kukimbia basi tutapeana taarifa na kujipanga kumkamata. Ni lazima tabia hii tuitokomeze" alisema Abdalah Chibidu mwendesha bodaboda wa kijiweni.
KWENYE PICHA NI MMOJA WA WAHALIFU WANAOTUHUMIWA KUIBA KWA PIKIPIKI